Vipengele
Dhima ya Ansible itasakinisha, usanidi na uendeshaji wa proksi inayojitegemea ya Snowflake.
- Msaada wa Ubuntu, Debian, Debian, Arch Linux, Fedora na FreeBSD.
- Kitengo cha Systemd cha kudhibiti huduma ya Snowflake kwenye GNU/Linux na hati ya rc ya FreeBSD.
Mahitaji
- Python
- Ansible 2.9 au juu zaidi
1. Sakinisha Ansible
Unaweza kusakinisha Ansible ukitumia pip
:
$ python -m pip install --user ansible
Au tafuta njia zingine ili kusakinisha Ansible.
2. Pakua jukumu la Ansible
Dhima ya Ansible inaitwa nvjacobo.snowflake
.
Unaweza kuipata ndani ya Hazina ya Galaxy na usakinishe kwa kutumia mstari wa amri:
$ ansible-galaxy install nvjacobo.snowflake
3. Unda kitabu cha kucheza
Kufuatilia, unda playbook ya Ansible ili kuendesha dhima mpya:
- hosts: snowflake
roles:
- nvjacobo.snowflake
4. Unda orodha
Hesabu ni orodha ya seva ambazo Ansible itadhibiti kiotomatiki kupitia kitabu cha kucheza.
[snowflake]
ip-address
5. Peleka/ Sambaza
Mwishowe, kwa kuendesha playbook, Ansible itapeleka proksi inayojitegemea Snowflake.
Unaweza kuiendesha kama root:
$ ansible-playbook -i inventory site.yml -u root
Au na sudo:
$ ansible-playbook -i inventory site.yml -u username -b
6. Dhibiti proksi ya Snowflake
Ikiwa mwenyeji wa proksi ya Snowflake inaendesha systemd, unaweza kudhibiti proksi yako ya Snowflake kwa kutumia amri za systemd: kuanza, hali na kuacha.
Kwa mfano:
$ ansible all -i inventory -a 'systemctl status snowflake-proxy'
Kwa FreeBSD, unaweza kudhibiti proksi yako ya Snowflake kwa kutumia amri hizi za maandishi ya rc.
Kwa mfano:
$ ansible all -i inventory -a 'service snowflake status'
7. Kuboresha proksi yako ya Snowflake
Ni muhimu kuweka proksi yako ya Snowfake inayojitegemea iwe imesasishwa.
Kuendesha playbook ya Ansible kutasakinisha masasisho:
$ ansible-playbook -i inventory site.yml -u root
8. (Si lazima) Kupunguza matumizi
Unaweza punguza idadi ya wateja (watumiaji wa Snowflake) kw kutumia client
.
Upeo wa juu wa wateja wanaotumia wakati mmoja kwa chaguo-msingi hauna kikomo (0 = isiyo na kikomo).
Playbook iliyopo hapa chini ina kikomo 300 ya wateja wanaotumia wakati mmoja:
- hosts: snowflake
vars:
clients: 300
roles:
- nvjacobo.snowflake
Kumbuka Kigezo hiki cha jukumu la Ansible kinachofaa hakipatikani kwa FreeBSD.