1. Wezesha usasishaji wa kiotomatiki wa programu
Mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuweka rilei yako salama ni kusakinisha masasisho ya usalama kwa wakati unaofaa na kiotomatiki ili usiweze kusahau kuihusu.
Fuata maelekezo ili kuwezesha usasishaji wa programu ya kiotomatiki kwenye mfumo wako wa uendeshaji.
2. Sanidi hazina ya mradi wa Tor
Kusanidi hifadhi ya mradi wa Tor kwa Fedora kimsingi inajumuisha kusanidi /etc/yum.repos.d/Tor.repo
na maudhui yafuatayo:
[tor]
name=Tor for Fedora $releasever - $basearch
baseurl=https://rpm.torproject.org/fedora/$releasever/$basearch
enabled=1
gpgcheck=1
gpgkey=https://rpm.torproject.org/fedora/public_gpg.key
cost=100
Habari zaidi juu yake inaweza kupatikana hapa.
3. Usakinishaji wa kifurushi
Sakinisha kifurushi cha tor
:
# dnf install tor
4. Faili ya Usanidi
Weka faili ya usanidi /etc/tor/torrc
mahali pake:
Jina la utani myNiceRelay # Badilisha "myNiceRelay" iwe kitu unachokipenda
ContactInfo your@e-mail # Andika barua pepe yako ukiwa unafahamu kuwa itachapishwa
ORPort 443 # Unaweza kutumia bandari tofauti ikiwa utataka
ExitRelay 0
SocksPort 0
5. Anzisha huduma
# systemctl enable --now tor
6. Maelezo ya mwisho
Ikiwa unapata shida kusanidi rilei yako tazama sehemu ya msaada wetu.
Ikiwa rilei yako inaendeshwa sasa angalia maelezo ya baada ya kusakinisha.