1. Sakinisha vifurushi vinavyohitajika
apt-get install unattended-upgrades apt-listchanges
2. Sasisha faili ya usanidi
Hii inachukulia kuwa utasanidi hazina ya kifurushi cha Tor Project kwa Debian/Ubuntu, ambayo imeandikwa hapa.
Weka mistari iliyo hapa chini kwenye faili ya usanidi /etc/apt/apt.conf.d/50unattended-upgrades
kila kitu ambacho kilikuwa ndani ya faili iliyotengenezwa kinaweza kuondolewa kabla ya kuongeza mistari iliyo hapa chini.
Debian:
Unattended-Upgrade::Origins-Pattern {
"origin=Debian,codename=${distro_codename},label=Debian-Security";
"origin=TorProject";
};
Unattended-Upgrade::Package-Blacklist {
};
Ubuntu:
Unattended-Upgrade::Allowed-Origins {
"${distro_id}:${distro_codename}-security";
"TorProject:${distro_codename}";
};
Unattended-Upgrade::Package-Blacklist {
};
Debian na Ubuntu
Sasisha faili /etc/apt/apt.conf.d/20auto-upgrades
na maudhui yafuatayo
APT::Periodic::Update-Package-Lists "1";
APT::Periodic::AutocleanInterval "5";
APT::Periodic::Unattended-Upgrade "1";
APT::Periodic::Verbose "1";
3. Anzisha upya kiotomatika
Ikiwa unataka kuwasha upya kiotomatiki ongeza yafuatayo mwishoni mwa faili /etc/apt/apt.conf.d/50unattended-upgrades
:
Unattended-Upgrade::Automatic-Reboot "true";
4. Tahini
Unaweza kujaribu usanidi wako wa uboreshaji ambao haujashughulikiwa na amri ifuatayo:
# unattended-upgrade --debug
Ikiwa unataka kuona matokeo ya utatuzi lakini usibadilishe chochote tumia:
# unattended-upgrade --debug --dry-run