1. Kupeleka chombo
Tunatoa faili ya kutunga docker inayokusaidia kupeleka kwenye chombo.
Kwanza, pakua docker-compose.yml alafu uandike usanidi wako wa kiungo kwa faili mpya.env
ambayo iko kwa saraka sawa na docker-compose.yml
. Hii hapa ni kiolezo:
# Kiungo chako cha bandari ya Tor.
OR_PORT=X
# Kiungo chako cha bandari ya obfs4.
PT_PORT=Y
# Barua pepe yako.
EMAIL=Z
Badilisha X
na bandari yako unayotaka AU, Y
na bandari yako yaobfs4 (hakikisha kwamba bandari zote zimetumwa kwenye ngome yako) na Z
na anwani yako ya barua pepe ambayo huturuhusu kuwasiliana nawe ikiwa kuna shida na kiungo chako.
Ukiwa na usanidi wa kiungo chako mahali sawa, sasa unaweza kupeleka chombo kwa kuendesha:
docker-compose up -d obfs4-bridge
Amri hii itapakia kiotomatiki faili yako ya docker-compose.yml
huku ikizingatia vigezo vya mazingira katika .env
.
Unapaswa sasa kuona matokeo sawa na yafuatayo:
Starting docker-obfs4-bridge_obfs4-bridge_1 ... done
Ni hayo tu! Kontena yako sasa kinafunga kiungo chako jipya cha obfs4.
2. Boresha chombo chako
Kuboresha kwenda kwa toleo jipya zaidi la picha yetu ni rahisi kama kuvuta toleo jipya zaidi la picha inayoendeshwa:
docker-compose pull obfs4-bridge
Na kisha kuanzisha tena chombo:
docker-compose up -d obfs4-bridge
Kumbuka kuwa saraka ya data ya kiungo chako (inayojumuisha nyenzo zake muhimu) imehifadhiwa katika kiwango cha docker kwa hivyo hutapoteza utambulisho wa kiungo chako unapopata picha ya hivi punde zaidi ya docker.
Ikiwa unaendesha viungo vingi katika kompyuta yako utahitaji kurudia hatua hii kwa kila kiungo.
Tutatangaza matoleo mapya ya picha kwenye tor-dev orodha ya kutuma barua.
3. Kufuatilia kumbukumbu zako
Unaweza kukagua kumbukumbu za kiungo kwa kuendesha:
docker logs CONTAINER_ID
Kutumia kiungo chako kipya kwa kivinjari cha Tor unahitaji "mstari wake wa kiungo".
Hii hapa ndivyo unavyoweza kupata mstari wa kiungo chako:
docker exec CONTAINER_ID get-bridge-line
Hii itarudisha kamba sawa na ifuatayo:
obfs4 1.2.3.4:1234 B0E566C9031657EA7ED3FC9D248E8AC4F37635A4 cert=OYWq67L7MDApdJCctUAF7rX8LHvMxvIBPHOoAp0+YXzlQdsxhw6EapaMNwbbGICkpY8CPQ iat-mode=0
Ikiwa una shida kusanidi kiungo chako angalia sehemu yetu ya usaidizi.
Ikiwa kiungo chako kinajiendesha sasa tazama maelezo ya baada ya usakini.
4. Matumizi ya hali ya juu
Unaweza kuweka vigezo vya ziada vya torrc katika faili yako ya .env
kwa kuweka OBFS4_ENABLE_ADDITIONAL_VARIABLES
hadi 1 na kuweka awali chaguzi za torrc zinazohitajika kwa OBFS4V_
. Kwa mfano, ili kuweka chaguo la AddressDisableIPv6
jumuisha mistari ifuatayo kwenye .env
:
OBFS4_ENABLE_ADDITIONAL_VARIABLES=1
OBFS4V_AddressDisableIPv6=1
Unaweza kupakua kiolezo chetu .envili kuanza.